COOL GIRL
This is a blog to view daily news as well collect opinions from different user
Saturday, June 9, 2012
TENGA AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE SAKATA LA YONDANI KUONDOKA KAMBI YA STARS KWENDA KUSAINI MKATABA YANGA
Saturday, June 9, 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KLABU
ya soka ya Simba imepokea kwa furaha taarifa kwamba Rais wa Shirikisho
la Mpira was Miguu Tanzania (TFF), Leodger Chila Tenga, ameagiza
kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na namna mchezaji wa Simba na Taifa
Stars, Kelvin Patrick Yondani, alivyoondoka kambini usiku wa kuamkia
Juni 7 mwaka huu.
Katika
barua ambayo Tenga ameiandikia Simba, ameahidi kwamba uchunguzi
utafanyika katika maeneo makuu mawili. Mosi, iwapo ni kweli Yondani
aliondoka kambini usiku, pili iwapo aliondoka kwa ruhusa maalumu au
alitoroka.
Tenga
ameahidi kwamba kama ikibainika kwamba aliondoka bila ruhusa, basi
hatua zitachukuliwa kwa wote waliohusika chini ya taratibu za maadili
kwa wachezaji (Players Code of Conduct).
Kutokana
na kauli hiyo ya Tenga, uongozi wa Simba umeamua sasa kwamba
hautozungumza lolote kuhusiana na masuala ya Yondani. Tayari timu
imewasilisha vielelezo vyake TFF na kote kwingine ambako suala hilo
linaweza kufika. Kilichobaki sasa ni kusubiri vyombo husika vifanye kazi
yake.
Simba
SC inapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wapenzi na wanachama wake
kutulia na kutobabaishwa na taarifa za wachezaji wake kusajiliwa na timu
nyingine.
Kwa
sasa Simba inaendelea na mikakati yake ya usajili unaokidhi vigezo vya
kimataifa ambao ulisababisha msimu uliopita itwae ubingwa wa Tanzania na
kuifunga YANGA goli 5-0 !
Simba si timu ya maneno mengi kwenye usajili bali ni vitendo.
Tunaomba
wanachama wetu watulie na mara ifikapo tareje 15 Juni mwaka huu, mbivu
na mbichi zote zitajulikana. Siku hiyo, Simba itatangaza wachezaji wake
wote iliyowasajili na iliyowaacha.
Simba
ndiyo mabingwa wa Tanzania na washabiki wake wanatakiwa kutembea vifua
mbele popote pale walipo na wasichanganywe na taarifa za pembeni.
Uongozi wa Simba uko makini na unafanya kazi zake kisayansi.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
KUELEKEA MCHEZO WA GAMBIA KESHO-POULSEN ALIA NA TFF
TIMU ya soka ya Taifa ‘Kili Taifa Stars’ kesho inashuka katika
dimba la Taifa jijini Dar es Salam kukwaana na Gambia ‘The Scorpions’ katika
mchezo wa mchujo wa kuwania kucheza fainali za kombe la dunia 2014
zitakazopigwa nchini Brazil.
Akizungumza na waandishi wa habari,kocha mkuu wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen alisema kikosi kikosi chake kipo katika hali
nzuri ya kimchezo ambao anaamini utakuwa na upinzani mkubwa.
Hata hivyo, Poulsen alisikitishwa TFF kutompatia DVD za mechi za Gambia
ili iweze kuwasaidia katika maandalizi ya mchezo wa kesho na kuongeza kuwa hii ni
mara ya pili kushindwa kupatiwa DVD hizo ambapo awali ilikuwa katika mchezo
dhidi ya Ivory Coast
ambapo Stars ililala mabao 2-0.
“Pamoja na kuzikosa DVD hizo nimekiandaa kikosi changu
kukabiliana na Gambia
ambapo naamini watatumia vizuri uwanja wa nyumbani kwa kushinda mabao
mengi,”alisema.
Poulsen aliongeza kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri
isipokuwa Nurdin bakari, huku kiungo mshambuliaji Haruna Moshi ‘Boban’
aliyekuwa majeruhi hali yake ikiimarika na huenda leo akampanga dimbani.
Hata hivyo mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa na ushindani
mkubwa na hasa ikizingatiwa kila timu inahitaji ushindi ambapo Gambia ilitoka sare ya bao 1-1 Morocco
na Morocco
katika mchezo wao ulipigwa nyumbani wiki iliyopita.
Kocha
wa Gambia,
Mtaliano Luciano Machini akizungumza jana katika mazoezi yao kwenye
uwanja wa Karume, alisema itakuwa ngumu kwa sababu wapinzani wao ni
wazuri na wana kasi uwanjani.
Mchezo
huo utakapigwa kuanzia saa 10.00 jioni na
kuchezeshwa na waamuzi kutoka nchini Zimbabwe, Ruzive Ruzive akisaidiwa
na Salani Ncube na
Edger Rumeck ambapo tiketi zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali
huku kesho zoezi hilo litahamia uwanja wa Taifa kuazia saa 6 mchana.
Viingilio katika mchezo huo ni sh.3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na
kijani, huku sh.5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, wakati VIP C watalipa sh.
10,000 , VIP B watalipa sh. 20,000 na
watakaokaa VIP A watalipa sh. 30,000.
AZAM FC KUANZA KUJINOA J'3
MABINGWA
wa kombe la Mapinduzi Azam Fc jumatatu ya keshokutwa inatarajiwa kuanza
kujinoa kwa ajili ya michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua
vumbi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi huu.
Msemaji wa msaidizi wa Azam Fc Jaffer Idd Maganga amesema kwamba wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kamni siku hiyo tayari kuanza mazoezi yao.
Azam Fc inayonolewa na Muingereza Stewart Hall, pia ni wa shindi wa pili wa ligi kuu soka Tanzabnia Bara
Msemaji wa msaidizi wa Azam Fc Jaffer Idd Maganga amesema kwamba wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kamni siku hiyo tayari kuanza mazoezi yao.
Azam Fc inayonolewa na Muingereza Stewart Hall, pia ni wa shindi wa pili wa ligi kuu soka Tanzabnia Bara
SAMATTA HUYOOOOO MAN CITY
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mbwana Samatta, huenda akajiunga
na mabingwa wa Ligi Kuu England, Man City.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinaeleza kwamba nyota huyo aliyeibukia Simba Sc kwa sasa yupo katika mazungumzo na mawakala wa Ulaya ili aweze kwenda kufanya majaribio Man City na hatimaye kujiunga nayo iwapo atafuzu majaribio yake.
Imeelezwa kuwa, mawakala hao wameshawasili Kinshasha, DRC na kuanza mazungumzo na uongozi wa klabu ya TP Mazembe kuhusina na nyota huyo ambaye pia anakipiga katika timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars.
Samatta alijuiunga na TP Mazembe akitokea Simba kwa dau la dola 200,000.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinaeleza kwamba nyota huyo aliyeibukia Simba Sc kwa sasa yupo katika mazungumzo na mawakala wa Ulaya ili aweze kwenda kufanya majaribio Man City na hatimaye kujiunga nayo iwapo atafuzu majaribio yake.
Imeelezwa kuwa, mawakala hao wameshawasili Kinshasha, DRC na kuanza mazungumzo na uongozi wa klabu ya TP Mazembe kuhusina na nyota huyo ambaye pia anakipiga katika timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars.
Samatta alijuiunga na TP Mazembe akitokea Simba kwa dau la dola 200,000.
JERRY TEGETE AIZODOA SIMBA SC
KLABU ya soka ya Yanga imewapiga tena bao la kisigino
mahasimu wao wa jadi nchini Simba baada ya kumuongezea mkataba wa miaka
miwili nyota wake Jerryson Tegete.
Wakati ligi kuu soka Tanzania Bara ikielekea ukiongoni,
Simba ambao ni mabingwa wa ligi hiyo walianza mpango wa kutaka kumsajili
mchezaji huyo baada ya kuwepo taarifa kutoka Yanga kwamba haina mpango naye
tena.
Hata hivyo, baada ya tetesi za Simba kumuwania Tegete kuzagaa
mtaani ndipo Yanga iliporudi nyuma na kuamua kumfunga mchezaji huyo ambaye
mkataba wake ulikuwa unalizika mwezi huu hadi mwaka 2014.
Mmoja ya wadau wa
Yanga wanaohusika na usajili wa wachezaji katika klabu ya Yanga alisema jana
kwamba wameamua kumbakiza kundini Tegete kutokana na umuhimu alionao katika
kikosi hicho.
“Napenda niwatoe shaka wanayanga kwamba kwa Tegete
ataendelea kuvaa uzi wa njano na kijani kwa miaka miwili…wale walikuwa
wakimuwania nawapa pole kwani ameshamwaga wino jangwani,”alisema.
Tegete ambaye msimu
uliopita hakuweza kung’ara alitua Yanga
mwaka 2008, akitokea sekondari ya Makongo, ambapo kutokana na umahiri alionao
kwa nyakati tofauti alipata kuichezea timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.
Yanga ambayo kwa sasa imeingia vita na Simba baada ya
kumsainisha mkataba wa miaka miwili nyota wake Kelvin Yondan ‘Vidic’, pia
imeshamsajili kipa wa Simba Ally
Mustafa ‘Barthez’ ikionekana kama kulipa kisasi baada ya Simba kumsajili Kiggi Makassy.
KHADIJA KOPA KUPAMBA MISS LAKE ZONE INTERCOLLEGE 2012
Malkia wa mipasho na mshindi wa tuzo za Tanzania Kili music
Awards 2012 Khadija Kopa anategemewa kuwa kivuto kikubwa kwa kutoa burudani ya
kipekee katika shindano la kumsaka mlimbwende wa MISS lAKE ZONE INTERCOLLEGES
2012 ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika mkoani Kagera katika mji wa Bukoba.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hii jijini Dar es salaam Mwandaaji wa shindano hilo
Bw.Joseph Rwebangira amesema kuwa asilimia kubwa ya maandalizi
yameshatimia,hata hivyo Rwebangira aliongezea kuwa mshereheshaji wa siku hiyo
atakuwa mchekeshaji maarufu afrika mashariki na kati Mpoki wa the origina
comedy.
Miss Lake zone
Intercolleges 2012 inayoandaliwa na kampuni ya Angles Real Entertainment ya
jijini Dar es salaam chini ya Mkurugezi wake Joseph Rwebangira imejipanga vya
kutosha kuleta mabadiliko ikiwa na lengo la kumfikisha mrembo wake katika ngazi
ya fainali kitaifa.
Shindano hilo
litafanyika katika ukumbi wa Linuz Club uliopo Bukoba mjini siku ya jumamosi
tarehe 23 juni ambapo mbali ya hayo
kutakuwa na burudani za ngoma za asili na wasanii wa mkoa wa Kagera,pia
kiingilio kitakuwa ni Tsh 10,000/= kawaida na V.I.P ni Tshs 15,000/=
YONDAN NUSURA ATIMULIWE STARS, TFF YAGOMA KUZUNGUMZIA SAKATA LAKE
BEKI
wa kati wa timu ya Simba Kelvin Yondan nusura atimuliwe katika kambi ya
timu ya Taifa baada ya kutoroka na kwenda kusaini mkataba na klabu ya
Yanga.
Habari kutoka kambi ya Stars iliyopo hoteli ya Tansoma katikati ya jiji la Dar es Salaam zinaeleza kuwa kocha mkuu wa Stars Kim Poulsen alimuweka kiti moto nyota huyo baada ya kubaini kuwa hakuwepo kambini usiku wa juzi, lakini baada ya kujitetea ndipo alipoamua kumsamehe.
Uongozi wa Simba kupitia mwenyekiti wake Alhaj Ismail Aden Rage umesisirtiza kuwa Yondan ni mchezaji wake halali na kwamba Yanga wamebugi step kumsainisha mkataba mptya.
Kama hiyo haitoshi, Rage alisema wanatarajiwa kufikisha suala hilo kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na lile la Kimataifa (FIFA) kwani hata mkataba wenyewe huo una utata katika baadhi ya vipengele, huku kiongozi aliyeshiriki kusimamia zoezi hilo si kiongozi halali wa Yanga.
Huku hayo yakiendelea, TFF kupitia kwa msemaji wake Boniface Wambura imeshindwa kuzungumzia juu ya sakata hilo na kuombwa lipewe nmuda kwanza ya kutafuta vielelezo kuhusina na mchezaji huyo ambaye amelamba kitita cha shilingi mil.30 kwa ajili ya kumwaga wino Yanga ambapo pia atakuwa akilambva mshahara wa sh.800,000 kwa mwezi.
Habari kutoka kambi ya Stars iliyopo hoteli ya Tansoma katikati ya jiji la Dar es Salaam zinaeleza kuwa kocha mkuu wa Stars Kim Poulsen alimuweka kiti moto nyota huyo baada ya kubaini kuwa hakuwepo kambini usiku wa juzi, lakini baada ya kujitetea ndipo alipoamua kumsamehe.
Uongozi wa Simba kupitia mwenyekiti wake Alhaj Ismail Aden Rage umesisirtiza kuwa Yondan ni mchezaji wake halali na kwamba Yanga wamebugi step kumsainisha mkataba mptya.
Kama hiyo haitoshi, Rage alisema wanatarajiwa kufikisha suala hilo kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na lile la Kimataifa (FIFA) kwani hata mkataba wenyewe huo una utata katika baadhi ya vipengele, huku kiongozi aliyeshiriki kusimamia zoezi hilo si kiongozi halali wa Yanga.
Huku hayo yakiendelea, TFF kupitia kwa msemaji wake Boniface Wambura imeshindwa kuzungumzia juu ya sakata hilo na kuombwa lipewe nmuda kwanza ya kutafuta vielelezo kuhusina na mchezaji huyo ambaye amelamba kitita cha shilingi mil.30 kwa ajili ya kumwaga wino Yanga ambapo pia atakuwa akilambva mshahara wa sh.800,000 kwa mwezi.
STORY OF THE WEEK
Are you a ware that mood swings and idiosyncratic behaviors of our workmates, friends and brothers may be a sign of mental disorder? George Adriano writes
When I set my eyes on
her, she looked away! Jolie is a beautiful young girl of 21 years old. She is
leading a single life after dropping out of school at form five. She is not
employed and stays with her grandparents
at Gongo la Mboto.
I failed to restrict myself
and said, “Talk to me baby!” She was shocked at my voice like someone from deep
thoughts, but she kept quiet. “I am sorry” I said. She didn’t answer anything
and instead walked away.
I decided to inquire from the other girl who
was standing next to me about this beautiful quiet girl. She was her elder Sister,
Nashie. “Is she dumb?” I asked. “No! She
is my young sister, her name is Jolie” Nashie replied. “Is she mentally okay?”
“Yes” “So what is wrong? Did I offend
her?” Mmh! Nashie was not sure but she told me a full story about Jolie.
Jolie was very okay
until three years earlier when she insidiously started being very shy. She avoided
walking together with other students and sometime covered her face with
clothes. Later on she did so even to her close family members.
After some months, she refused coming out of her room and she was looking at herself in a mirror complaining that she looked ugly with ‘a big nose’ and that other people will laugh at her. She ended up breaking the mirror. She was very irritable when forced to come out of her room.
Later she also
developed insomnia. Sleeping at midnight and getting up very early at around 4.00
a.m and remaining a wake on the bed. Strange enough, she even spent most of the
day time in the bedroom not actually sleeping but engrossed in her own thoughts.
She also lost appetite, ate with difficulties ending up into food wastage as
noted by her relatives.
It took her a year, and
then she completely refused to go to school. She lost interest in various daily
activities like cooking, watching TV or fetching water claiming that all these
were boring and life was not good.
Two years before, their
father had died after being involved in a tragic road accident with a motorcycle,
Jolie felt very sorrowful and spent most
of the days and nights thinking about
her father.
In the same year,
something happened to Jolie, when she was fetching some water from a shallow
well, a stone throw distance from home
at around 8:00 pm, a middle aged man abused her sexually (forcefully, he had unprotected
sex with her). She narrated the story to her relatives, but no action was taken
against the perpetrator, she felt very bad but she was unable to do anything. Consequently,
she has been experiencing lower abdominal pains even when not in menses.
I told my friend who is
a doctor, about Jolie, the girl whom I loved so much. This was his response;
Doctor:
Does your friend Jolie have a big nose?
Me:
Aah No! She has a small really cute nose, I admire it.
Doctor:
Jolie might be suffering from mood disorders. Mood disorders involve the
disabling of the emotions. It is
convincing that, Jolie has Major Depressive Disorder (MDD), which is one of the
mood disorders. She may also have somatoform disorder as she thinks that she
has a big nose. The doctor offered me a
cold yet insightful analyses of mental disorders which opened my understanding
with regards to Jolie.
He explained that depression
is an emotional state characterized by,
·
Sadness
or loss of connection with the ordinary world
·
Feelings
of worthlessness and guilt. You may not think that you are a valuable person
which leads to having low self esteem.
·
Withdrawal
from others. you isolate yourself.
·
Lack
of sleep; You don’t fall asleep though you may need to sleep
·
Reduced
or loss of appetite.
·
Lack
of sexual desire. The victim may erect and perform but minus the usual
testosterone triggered urge
·
You
may attempt or think to commit suicide, arguing that it’s better to die rather
than to live
·
Inability
to concentrate which occurs nearly every day.
·
Depression
impairs important normal functions (such as work or personal relationships).
·
Drugs,
alcohol, or other substances do not cause them.
When these conditions
persist for two weeks (14 days) or more, then it is a Major Depressive
Disorder. A person loses interest in most of the things or activities she/he
used to enjoy. It is mostly prevalent among people of above 25 years. The
duration and the severity of the symptoms vary. The likely cause of the ailment
depends on several factors: a manifestation of a previous mental illness to the
individual and sometimes having a relative who has ever suffered from the same
(genetics) poor social support, poor adherence to the medication .However, faith
in God can help to deal with mental disorders whereby the patient surrenders to
the divine providence. A good job or a healthy relationship which you enjoy can
also immunize someone against them.
Me:
My God! Is it a mental problem?
Doctor:
Oh, yes. It’s a psychological condition but as you can see it may affect the social,
economic and spiritual life of a person.
Me:
I am finished. Okay, thank you, bye!
Doctor:
Hey! Sit please! I have not finished. This condition is curable. There are
several ways of helping your friend which will undoubtedly restore her former
self and you will go on enjoying life with her
Medication is among the
modalities of treating Major Depressive Disorder. The medical treatment is
usually accompanied by Psychological, social and even spiritual therapy. It’s
quite common for the symptoms to diminish and then appear again after a period
of time.
Me:
Huuu! What should I do?
Doctor:
It’s better to take your friend to the mental health professionals; clinical
psychologists, and a psychiatrist. It’s very important to adhere to the
medication in terms of dosage and duration, and make follow up to the mental
clinic. Consult your doctor for any adverse changes which Jolie may notice in
the course of treatment.
Me:
Okay, thank you very much. Bye
When I was just about
to shut the door and walk out, the doctor reminded me not to forget testing for HIV/Aids both of us, and pregnancy
test for Jolie.
Written
by;
Mwitha Thomas
Computer science student at UDSM
Mob:
+255 714689297
Thursday, June 7, 2012
TANGAZO LA MKUTANO WA HADHARA WA CHAMA CHA MAPINDUZI UTAKAOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI, SIKU YA JUMAMOSI, TAREHE 09-06-2012.
TANGAZO:
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kimeandaa
Mkutano Mkubwa wa Hadhara kwa wananchi wote, Siku ya Jumamosi, tarehe
09/06/2012, Katika Viwanja vya Jangwani Kuanzia saa 8 mchana.
Maudhui; “ Kutoa Msimamo Wake Juu
ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa. Hivyo Chama Kitatumia Fursa hiyo
Kuelezea Watanzania Juu ya Msimamo Wake Katika Mambo yafuatayo:
1.
Hatma ya maisha ya Watanzania
·
Ajira
·
Miundo mbinu ya Barabara, Reli,
Bandari Na Anga.
·
Bei za bidhaa
mbalimbali.
·
Umeme
·
Rasilimali za taifa
2.
Msimamo wa Chama Cha Mapinduzi kuhusu
Mchakato wa Katiba Mpya.
3.
Vurugu za Zanzibar.
Katika Mkutano huo, Viongozi
mbalimbali wa Chama na Serikali watakuwepo na kutoa ufafanuzi juu ya masuala
hayo yaliyoainishwa kama msimamo wa Chama Cha Mapinduzi.
Chama Cha Mapinduzi, kinawaalika
wanachama wake wote, wakereketwa na wananchi kwa ujumla kuhudhuria katika
mkutano huo mkubwa. Mkutano utafanyika kwa amani na utulivu na wote
mnakaribishwa.
KIDUMU CHAMA CHA
MAPINDUZI
Imetolewa na:
JUMA SIMBA
KATIBU WA SIASA NA
UENEZI
MKOA WA DAR ES
SALAAM.
07/06/2012
JAMAA WAKUTANA NA ADHA YA WANAJESHI ALMAARUFU KAMA WAJEDA.
Kila siku mnaambiwa msipite maeneo yao hawa jamaa lakini raia hamkomi.
wanajeshi
walivyo msuba.............inaweza ndio ikawa shughuli ya siku
nzima.........mkacheza kiduku hapooo hadi maji
yatakapokauka............h awana tatizo na mtu, watapeana zamu ya kwenda kula ila raia ndio mtakausha huo Mto.
KCB TANZANIA YAZINDUA HUDUMA MPYA YA DISPORA BANKING
Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania DK Edmund
Mndolwa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya KCB DIASPORA
BANKING uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund
Mndolwa, akizindua rasmi huduma mpya inayotolewa na KCB DIASPORA BANKING,
Katikati ni Mmoja wa Mameneja wa benki hiyo SHOSE KOMBE. Anayeshuhudia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo MOEZ MIR.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki
ya KCB Tanzania wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa huduma mpya ya KCB DIASPORA
BANKING iliyoanzishwa na benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na
Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania Christine Manyenye akifafanua kuhusiana na
huduma mpya iliyoanzishwa na benki hiyo ya KCB DIASPORA BANKING wakati wa hafla
ya uzinduzi iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki
ya KCB Tanzania wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa huduma mpya ya KCB DIASPORA
BANKING iliyoanzishwa na benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanyika leo
Jijini Dar es Salaam
Sakata la Mafuta Jijini Mbeya: Mafuta ya Taa Jijini Mbeya ya panda bei kutoka Tsh 2175 mpaka kufikia Tsh 3000 na 3500. Ni Kutokana na uhaba wa Mafuta hayo.
Wananchi
wa Jiji la Mbeya wakiwa wana haha kupata Mafuta ya taa katika kituo cha
mafuta
Baadhi
ya Njinga zikiwa zimepaki eneo ambalo ndilo pekee Mafuta yanapatikana jinini
Mbeya
Mdau
akiwa anatazama vema kama anazo pesa za kununua Mafuta hayo baada ya kushtuka
kuambiwa kuwa bei imepanda mpaka kufikia 3500
Kila
mtu anataka kupata mafuta kwa muda katika eneo hilo Mpaka wenye mapipa nao
wamo.
KITUKO KUTOKA KWENYE AKAUNTI YA FACE BOOK YA JOHN KITIME LEO!
Mwanamuziki nguli John Kitime
Joji alikuwa shule ya vidudu na akaanza kujua hesabu. Mjomba wake akaja;
JOJI: Mjomba najua hesabu.
MJOMBA: Tatu kujumlisha mbili?..Mtoto akaanza kuhesabu vidole akamaliza;
JOJI: Tano
MJOMBA: Haya sasa sitaki uhesabu vidole. Tia mikono yako kwenye mifuko ya kaptura. Haya tano kujumlisha tano?....mtoto akaanza kuhesabu vidole mfukoni.
JOJI: Kumi na moja!!
JOJI: Mjomba najua hesabu.
MJOMBA: Tatu kujumlisha mbili?..Mtoto akaanza kuhesabu vidole akamaliza;
JOJI: Tano
MJOMBA: Haya sasa sitaki uhesabu vidole. Tia mikono yako kwenye mifuko ya kaptura. Haya tano kujumlisha tano?....mtoto akaanza kuhesabu vidole mfukoni.
JOJI: Kumi na moja!!
Haaaa haaaa haaaa haaaaa!!!! Joji you are Very Bright!
KAMATI ZA BUNGE ZAENDELEA NA KAZI YA KUPOKEA MAKADIRIO YA BAJETI ZA WIZARA LEO
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzo Mhe. Shukuru Kawambwa akiwasilisha makadirio ya
bajeti ya Wizara yake mbele ya Kamati ya Huduma za Jamii kabla ya kupelekwa
Bungeni. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Mhe. Magareth Sitta na
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.
Makamu
Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Jamii Mhe. Faustine Ndugulile (kushoto) na
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Magareth Sitta (katikati) wakimsikiliza kwa
makini Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzo Mhe. Shukuru Kawambwa alipokuwa
akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake mbele ya kamati hiyo
leo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Jenister Mhagama akisisitiza jambo
wakati wakipokea makadirio ya bajeti ya wizara ya kazi na Ajira iliyo wasilishwa
mbele ya kamati hiyo. Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.
Juma Nkamia na Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Chacha Nyakega, Waziri wa Kazi na
Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka na naibu waziri wa Wizara ya kazi na Ajira Mhe. Dkt
Milton Makongoro Mahanga.
Mwenyekiti
wa Kamati ya fedha na Uchumi Mhe. Andrew Chenge akifafanua jambo mbele ya
wajumbe wakamati na watendaji kutoka wizara ya fedha baada ya kupokea
mapendekezo ya bajeti ya wizara ya fedha yaliyo wasilishwa mbele ya kamati hiyo
leo. Kulia kwake ni Waziri wa fedha Mhe. William Mgimwa Mhe Saada Mkuya Salum na
Mhe Janet Mbene, amabo ni Manaibu waziri katika wizara hiyo.
Mjumbe
wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma Mhe.Murtaza Ally Mangungu akifurahia
jambo baada ya kupokea hesabu zilizokaguliwa za chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)
kwa mwaka 2010/2011. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. zitto Kabwe
na Kushoto ni Katibu wa Kamati hiyo Erick Maseke
kamati
ya POAC ikiendelea na kazi.
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge
AUWA NA KISHA KUNYOFOLEWA UUME, NA MIKONO MKOANI ARUSHA
KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA ARUSHA LIBERATUS SABAS
(NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA)
Mtu mmoja ambaye hajajulikanan jina lake
amefarikidunia huku baadhi ya viungo vyake hasa sehemu za uume wake
zikiwa zimechomolewa pamoja na mikono yake
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa
arusha Sabas Liberatus alisema kuwa tukio hilo lilitokea may 26 majira
ya saa tni asubuhi katika eneo la Mto Nambala wilyani Arumeru
Kamanda Sabas alisema kuwa katika siku ya tukio mytu mmoja mwenye
jinsia ya kiume ambaye hajatambulika mpaka sasa anakadiriwa kuwa na
miaka25-30 alikutwa akiwa amefariki
Kamanda huyo aliongeza kuwa mara baada ya wapita njia kumkuta
akiwa amefariki waligundua kuwa pia hana viungo mbalimbali ndani ya
mwili wake hali ambayo ilizua tafrani kubwa
‘hawa watu walipomuangalia kwa undani sana waliweza kujua na
kutambua kuwa baadhi ya viungo vyake havipo na ndipo walipota taarifa
kwa jeshi la polisi na sisi tulipoofika ndani ya eneo la tukio
tuliyakuta hayo hayo”alisema Kamanda Sabas
Pia aliongeza kuwa baada ya polisi kufika katika eneo la tukio walikuwa
mwili huo ukiwa na suruali aina ya jeans ambayo ilikuwa imeshushwa hadi
chini ya magoti na viungo vyake vikiwa vimenyofolewa
Hataivyo
jeshi hilolinaendela na upelelezi juu ya tukio hilona upelelzi wa
kumfahamu chanzo cha umati huo huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mount Meru
Waziri akizungumza na Kamati ya Bunge
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa
akizungumza na Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira kwenye
ukumbi wa Hazina kulia Mwenyekiti wa Kamati hiuo James Lembeli kushoto
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga,Naibu katibu Mkuu
Eng Ngosi Mwihava,Mh Zakhia Megji kikao hicho kimefanyika leo Mjini
Dar es Salaam[Picha na Ali Meja
Baraza la Sanaa (BASATA) lawapa somo waandaaji wa Epic Bongo Star Search 2012
Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina
ya siku moja kwa majaji wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka
kuzingatia maadili ya kazi zao.
Akitoa somo kwa majaji hao mratibu wa matukio wa
Basata Malimi Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa asilimia kubwa
ya washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza
vipaji.
Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira
waliyotoka washiriki na kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa
kuwa wapo ambao wana vipaji lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea
mazingira.
Alisema kuwa kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu
washiriki wa miaka 16 hivyo ni vema zaidi wakazingatia suala la sauti kulingana
na umri wa mshiriki sababu watakuwepo wenye sauti za kitoto
pia.
Pia aliwataka majaji hao kuhakikisha kuwa hawatoi aina
yoyote ya upendeleo na wala kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano
hilo.
Pia alisisitiza kuwa majaji wanalo jukumu kubwa la
kuwaelekeza namna ya kuimba, kuvaa, kujiheshimu na usafi wa mwili
pia.
“Hiii ni semina ya kuwekana sawa tu kwa kuwa hili
shindano lipo kwa muda mrefu na majaji mmekuwa mkifanya vema, kwa niaba ya
BASATA napenda kuchukua muda huu kuwataka muwe makini katika kuzingatia maadili
haya niliyoyasema na hata mengine pia”alisema Mashili.Naye Mkurugenzi wa
Berchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen alisema kuwa semina
hiyo ni muhimu kwa majaji kwa kuwa muda mzuri wa kukumbushana
mambo muhimu yahusuyo muziki.
Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani
Dodoma Juni 16 katika ukumbi wa Royal Village.
Majaji wa shindano hilo waliohudhuria ni pamoja na
Jaji Mkuu Ritha Paulsen, Master Jay, Salama pamoja na mratibu wa
EBSS kutoka Basata Vicky Temu.
habari zaidi ingia
www.elimuboratanzania. blogspot.com
MWENYEKITI WA KLABU YA SIMBA ASEMA: MKATABA WA YONDAN YANGA NI BATILI
Simba Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans
kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patric
Yondani kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana
wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya
Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young
Africans.
Kwamba katika picha hiyo ameonekana mjumbe wa Young aliyejiuzuru
bwana Seif Ahmed na hilo lilitoa shaka kama utaratibu huo umefanywa na
klabu ya Young, lakini shaka hiyo imeondolewa pale ambapo tovuti ya
Young imetangaza kumsajili mchezaji huyo wa Simba SC, lakini zaidi ya
hilo picha inaonyesha fedha zikiwa zimewekwa mbele ya mchezaji jambo
linaloonyesha mazingira ya kurubuniwa kwani kwa utaratibu wa kifedha,
pesa nyingi kiasi hicho malipo yake yanashauriwa/yanapashwa kupitia
benki.
Mbali ya hayo picha hiyo inamuonyesha Kelvin akiwa katika jezi ya
mazoezi ya timu ya Taifa na yenye logo ya Kilimanjaro na kumbukumbu
zinaonyesha mkataba kati ya TBL na TFF tarehe 9/5/2012, kwa haraka
haraka tukio hilo limefanyika katika kipindi chini ya mwezi mmoja ingawa
taarifa za ushahidi zinaonyesha tukio hilo limetokea jana tarehe
6/6/2012.
Simba Sports Club ilipenda kuamini kwamba tukio hilo haliihusu
klabu ya Young kwani bwana Seif Ahmed alishajiuzuru kutoka kwenye kamati
ya Young Africans, kwani Young ni klabu kongwe na inayojua taratibu
zote za usajili.
Kwamba Simba Sports Club imeshawasiliana na jopo lake la mawakili
na inajiandaa kuishtaki klabu ya Young katika chombo husika cha mpira na
kudai adhabu ya kutopitisha majina yote ya usajili ya Young kwa mwaka
2012/2013 na miaka mingine miwili ijayo na Simba SC ipo tiyari
kufuatilia suala hili hadi katika mahakama ya mpira ya FIFA.
Kelvin Yondani ni mchezaji halali wa Simba Sc aliye na mkataba
hadi 31 mei 2014 mkataba ulioongezwa tarehe 23/12/2011 kuundeleza
mkataba wa awali uliokuwa unaisha tarehe 31/5/2012. Sheria za FIFA za
hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi katika kipengele cha 5 kifungu
kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja
tu kwa wakati mmoja.
Imetolewa tarehe 7/6/2012.
MH. ISMAIL ADEN RAGE (MB)
MWENYEKITI
SIMBA SPORTS CLUB
Rais Dk. Shein akutana na Balozi wa Msumbiji na Sweden
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali
Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania Amour
Zakaria aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,kwa kumaliza muda
wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania Amour
Zakaria aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,kwa kumaliza muda
wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali
Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania Amour
Zakaria aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,kwa kumaliza muda
wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania Amour
Zakaria aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,kwa kumaliza muda
wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Sweden Nchini
Tanzania Lennarth Hjelmaker,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar
kujitambulisha kwa Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Sweden Nchini
Tanzania Lennarth Hjelmaker,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar
kujitambulisha kwa Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini
Tanzania Lennarth Hjelmaker,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar
kujitambulisha kwa Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini
Tanzania Lennarth Hjelmaker,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar
kujitambulisha kwa Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
GAMBIA KUWASILI LEO USIKU TAYARI KWA MPAMBANO WAO NA TAIFA STARS
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa
iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili
leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi
dhidi ya Taifa Stars.
The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku
lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi
Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es
Salaam.
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza
mpira wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire
iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.
Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou
Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa
Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na Demba
Savage.
Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou
Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa,
Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na
Saloum Faal.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti Wa CUF Profesa ibrahim Lipumba Wahudhuria Mazishi Ya Mwenyekiti Mstaafu Wa CUF Marehemu Musobi Mageni
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akitoa salaam
za pole kwa viongozi na chama cha Wananchi CUF na wananchi wa mkoa wa
Mwanza katika mazishi ya Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, marehemu
Musobi Mageni
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiweka udongo kwenye kaburi la
Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, marehemu Musobi Mageni ,kulia kwake
ni Mwenyekiti wa Cuf Profesa ibrahim Lipumba ambao wote walijumuika
na viongozi na chama cha Wananchi CUF na wananchi wa mkoa wa Mwanza
katika mazishi ya Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, marehemu Musobi
Mageni
--
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amejumuika na
viongozi wa chama cha Wananchi CUF na wananchi wa mkoa wa Mwanza katika
mazishi ya Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, marehemu Musobi Mageni
huko kijijini kwao Ngudu, Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Katika mazishi hayo, pia alihudhuria Mwenyekiti wa chama hicho,
Profesa Ibrahim Lipumba, Makamu Mwenyekiti, Machano Khamis Ali, pamoja
na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa, wakiwemo Waziri wa Afya
Zanzibar, Juma Duni Haji na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Haki za
Binaadamu, Salum Bimani.
Marehemu Musobi alifariki Dunia Mei 30, mwaka huu nyumbani kwake
Ngudu baada ya kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo na damu na sukari
kwa muda mrefu.
Marehemu alihamia chama cha Wananchi CUF mwaka 1994 na
kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Taifa mwaka 1995 hadi 1999 alipostaafu na
kubaki kuwa Mjumbe wa kudumu wa Baraza Kuu la Taifa na Mkutano Mkuu wa
chama hicho hadi kifo chake.
Katika uhai wake, marehemu aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo Mijini kuanzia mwaka 1972 hadi 1975, mwaka 1976 hadi 1978
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Rajan Industries Ltd. Nafasi nyengine
ni alizowahi kushikilia ni Ubunge na Mkuu wa Wilaya katika wilaya ya
Chunya, Kahama na Muleba.
Akitoa salamu za rambirambi, Makamu wa Kwanza wa Rais, ambaye pia
ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
wakati wa mazishi alisema, marehemu alikuwa kisima cha busara na mwenye
hekima kubwa na ndio maana viongozi wa CUF walikuwa wakikimbilia kwake
kuchota ushauri wake.
“Huu ni msiba mkubwa sio tu kwa familia yake, bali kwa chama chetu na kwa serikali zote mbili”, alisema Maalim Seif.
Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1930, ameacha wajane wawili, watoto 15, wajukuu 28 na vitukuu sita.
Na
Khamis Haji
Ofisi Ya Makamu wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
MILIONI 421.8 ZAPATIKANA KUCHANGIA MPANGO WA ELIMU KATA YA KIPAWA JIJINI DAR ES SALAAM
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya
kuchangia mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata hiyo Bonah
Kaluwa, wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye
alikuwa mgeni rasmi kuingia ukumbini Katika hafla iliyofanyika jana
usiku ndani ya hoteli ya Kilimanjaro (Kempiski hotel) jijini Dar es
Salaam .
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Mgeni rasmi wa Hharambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa
kampuni ya Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma
baada ya kuchangia sh. milioni 22.
Mkurugenzi wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi
mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi
wa harambee hiyo.kushoto meneja
rasilimali Songas Bi Agatha Keenja.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja
(katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya
kuchangia sh. 500,000.
eya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa
elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Fedha hizo
zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400
zilipatikana.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendeleza kuwa mstari wa mbele
katika harakati zake za kuchangisha mamilioni ya fedha baada ya
kuchangisha Sh.421,850,000 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya
Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM), aliendesha harambee hiyo juzi
katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Kempiski Jijini Dar es Salaam
ambapo yeye mwenyewe alichangia Sh.milioni 10.
Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa
ni Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22, African
Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line
ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja
alichangia milioni Sh.10.
Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi,
Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds
walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh.
milioni 12.
Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha
wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu.
Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa jitihada
zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani wengine
kuiga mfano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwaupande wake alisema shule
saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na matatizo
lukuki ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha
wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja.
“Shule za kata yangu kwa kweli zinakabiliwa na changamoto nyingi, kwa
mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane
wakati wanafunzi waliopo ni 2,200, Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu
madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa.
Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa
ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa
matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15
kilichangwa na wadau mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3
zilitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group
ambao walitoa shilingi milioni moja na wanafunzi kadhaa wa shule za
msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau
waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na
kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na
matatizo hayo katika shule mbalimbali
Tawi la CHADEMA Washington DC Nchini Marekani Lazidi Kuvuna Wanachama Wapya
Linda Bezuidenhout (LB) furaha baada ya kuvua kamba kuvaa kwanda na kuchukua kadi kuwa mwanachama kamili wa Chama Cha Demokrasia Chadema.
Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA
Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe
Mwang'ombe akimkabidhi rasmi mwanacham mkareketwa ambae ni mwana
mitindo Linda Bezuidenhout (LB) kati ya uwanachama wa chama cha
Demokrasia Chadema katika ofisi ya tawi la Tawi la Chama Washington
DC.
Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington
DC Kalley Pandukizi akiwa na katibu wachama hicho,Ndugu Libe Mwang'ombe
alipotoa kadi rasmi kwa Beautician maharufu na designer wa kitanzan
Linda Bezuidenhout (LB)
Viongozi wa tawi la chadema Washington DC wakipata Champagne
Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA
Washington DC Mhe. Kalley pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe
wakipata picha ya pamoja na Linda Bezuidenhout Atlanta, Georgia na
wanachama wa tawi la chadema Washington DC.
Katika
miaka ya nyuma Linda aliwahi kusponsor matukio mbali mbali kwenye
miaka ya 1990 wengi wao wakimjua kwa Linda Express Nchini Tanzania
ambae ambaye hivisasa anajishughulisha na biashara ya nguo za kiume milanovita.com pamoja na zakike ambazo anadesign mwenyewe kwa brand name ya Linda kutoka Atlanta, Georgia Nchini Marekani.Picha na Mdau Wa Swahilivilla
TANGAZO LA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA :UPOTEVU WA VITABU ISHIRINI (20) VYA LESENI YA BIASHARA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa inapenda kuutangazia Umma kuwa imepotelewa na vitabu ishirini (20) vya leseni za biashara vilivyopotea tarehe 22 Mei 2012 katika moja ya Daladala Jijini Dar es Salaam.
Vitabu hivyo vilivyotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara vikiwa na kumbukumbu namba 1389501 mpaka 1391500.
Kwa yeyote atakayeona vitabu hivyo au kuvinunua anaombwa avipeleke kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake au kutoa taarifa juu ya mwenye navyo katika kituo hicho.
Ifahamike kuwa vitabu hivyo ni batili hivyo haviruhusiwi kutumika kwa namna yeyote ile. Na atakayethibitika kuvitumia atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
Ewe mfanyabiashara, epuka manunuzi na matumizi ya vitabu vyenye namba tajwa hapo juu kwa usalama wa biashara yako.
Kwa mawasiliano tunaomba mtumie namba zetu hapo juu.
Tunaomba ushirikiano wenu.
IMETOLEWA NA
HAMZA TEMBA
AFISA HABARI MKOA WA RUKWA
07/06/2012
YONDAN AKIMWAGA WINO YANGA NA KITITA CHAKE CHA MIL.30
KELVIN
Patrick Yondan, beki wa kati wa Simba amekana kusaini mkataba wowote na
Simba na amesema yeye amesaini Yanga tu mkataba wa miaka miwili.
Yondan amesema Simba wanampakazia kusaini mkataba mpya na anataka wapenzi wote wa soka Tanzania watambue kwamba kuanzia sasa yeye ni mchezaji halali wa Yanga.
Yondan aliikana Yanga awali kwa sababu walimsainisha fomu bila kumpa fedha, lakini leo amepewa Milioni 30 zake taslimu na amemaliza kila kitu.
Yondan amesema Simba wanampakazia kusaini mkataba mpya na anataka wapenzi wote wa soka Tanzania watambue kwamba kuanzia sasa yeye ni mchezaji halali wa Yanga.
Yondan aliikana Yanga awali kwa sababu walimsainisha fomu bila kumpa fedha, lakini leo amepewa Milioni 30 zake taslimu na amemaliza kila kitu.
Kwa hisani ya www.mamapipiro.blogspot.com
TIKA itaboresha huduma Ilala- Meya wa Ilala Jerry Slaa
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Slaa akufungua
semina ya Mpango wa bima ya Afya unaojulikana kama TIKA uliobuniwa na
Mfuko wa Bima wa Afya (NHIF) inayotolewa kwa madiwani wa Manispaa hiyo
inayofanyika kwenye ukumbi wa Arnautoglo Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam asubuhi hii, kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa NHIF Bw Khamis Mdee
na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ellias Mwasabwite.
Naibu Mkurugenzi wa NHIF Bw Khamis Mdeeakizungumza katika semina hiyo
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ellioth Mwasabwite na
katikati ni Meya wa Ilala Mh. Jerry Slaa.
Wakurugenzi na maafisa kutoka Mfuko wa Bima wa Afya wakiwa katika semina hiyo leo.
Madwani wanaoshiriki katika semina hiyo wakifuatilia kwa makini mada katika semina hiyo.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Slaa kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa
NHIF Bw. Khamis Mdee na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
Ellias Mwasabwite.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Slaa kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa
NHIF Bw. Khamis Mdee na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
Ellias Mwasabwite.
Subscribe to:
Posts (Atom)